Sunday, September 18, 2011

Kutuma na kupokea SMS kupitia kwenye intaneti.

BAADA ya simu nyingi kuwa zimekwishaandikishwa ni ujinga kuzuia watu kutumiana SMS kupitia kwenye kompyuta zao.

Teknolojia hii inatufosi kuwaachia watumiaji wa intaneti kuandika kwa urahisi na bila usumbufu SMS kwenye kompyuta na kisha papo kwa kubonya dirisha-tumizi linalohitajika kuibandika SMS hiyo na kishaa baada ya kuweka namba za simu husika kuituma bila kugusa simu yako ya mkononi.

Hili ni jambo muhimu kuwapunguzia wafanyakazi wanaotumia sana simu zao kuendelea kuitumia simu bila sababu yoyote muhimu wakati wanaweza kuitumia kompyuta.

Chaji au gharama za kutuma na kupokea simu zinaweza kutoka kwa yoyote yule, yaani, kati ya mtumaji na mtumiwaji, baada ya kifungu kidogo tu cha sheria kutahadharisha juu ya fursa kama hiyo.

Mobile Pesa na Akaunti za muda za Vikundi vya Kijamii na Kiuchumi

Biashara nyingine katika teknohama ni ile ya kuruhusu vikundi mbalimbali ambavyo havijaandikishwa rasmi kama vyama, kuwa na temporary account kupitia biashara za Mobile Pesa.

Kikundi kikishapata idadi ya wanachama fulani na huku kinaendelea kutafuta wengine na kujipanga kinaweza kuanzishiwa akaunti hiyo ili kusaidia kujenga imani kwa wanachama watarajiwa kwamba fedha zao ziko mahala salama na haziwezi kuliwa na mtu kirahisi bila kujulikana.

Monday, June 29, 2009

Ulaya sasa kuwa na aina moja tu ya chaja !

UMOJA WA ULAYA umeamua kwamba kuanzia sasa Ulaya yote itakuwa inatumia aina moja tu ya chaja katika kuchaji simu za mkononi.

Uamuzi umefuatilia usumbufu watu wanaoupata katika kutafuta ainay ya chaja inayofaa simu fulani. Matokeo yake ni kwamba kila mwaka mamilioni ya chaja zinazokufa hutupwa na hivyo kuongeza uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira duniani.

Kuwepo kwa chaja moja kutapunguza sana wingi wa chaja majumbani, mahotelini, vilabuni, vyuoni, maofisini na sehemu zingine mtu anazolazimika kuwa na chaja.

Chaja mbili tatu zitatosha kabisa zinapokuwepo sehemu husika na wote watakuwa wanachangia ubora wa mazingira yao.

USHAURI: Jadili na wenzako, je, chaja aina moja inahitajika hapa Afrika Mashariki ?

Saturday, June 27, 2009

Sanduku la Kura la Elektriniki

Sanduku la Kura la elektriniki litakuwa ni sanduku la kura sio tu linalopokea kura zilizopigwa na kuingizwa bali litakuwa na uwezo wa kusoma dole gumba la mpiga kura na kukubali au kuikataa kura yake kutokana na namba yake kutoendana na alama ya dole gumba lake. Ili kumpa nafasi ya pili, sanduku litaweza kumuuliza mtu neno lake la siri na akifanikiwa kuliingiza kura yake itakubaliwa. Aidha, sanduku hilo litaweza kumpiga picha mtu na kuoanisha na picha yake katika 'chipu' iliyoko kwenye sanduku hilo zikioana hali kadhalika kura yake inakubaliwa.

Sanduku hilo litakuwa linahesabu kura kiouto na kupeleka majibu kwa muda uliopangwa kutokea kwenye video itakayokuwa kwenye eneo la kupigia na kuhesabu kura. Kwa namna hii litakuwa linaondosha haja ya binadamu kuhesabu kura.

Uzuri wa masanduku ya elektroniki ni kwamba ni nchi moja tu inayostahili kuwa nayo. Na nchi yoyote inayofikia kipindi chake cha uchaguzi inaweza kuyaazima kutoka kwa nchi hii. Kutokana na miaka yake na sifa yake katika demokrasia ningelipendekeza India ndio wawe watengenezaji na na wakodishaji wa masanduku hayo.

Kutokana na kurahisisha kazi masanduku elektroniki yatarahisisha pia upigaji kura wakati wowot na mahala popote.

Endapo sanduku la kura elektroniki litakuwepo demokrasia itakuwa imekwepa vigingi vingi vinavyowekwa na wale wasiotaka kuiheshimu na kuienzi na kuwa wakweli, wanaowajibika na watenda haki kwa wanajamii wenzao.