Saturday, June 27, 2009

Sanduku la Kura la Elektriniki

Sanduku la Kura la elektriniki litakuwa ni sanduku la kura sio tu linalopokea kura zilizopigwa na kuingizwa bali litakuwa na uwezo wa kusoma dole gumba la mpiga kura na kukubali au kuikataa kura yake kutokana na namba yake kutoendana na alama ya dole gumba lake. Ili kumpa nafasi ya pili, sanduku litaweza kumuuliza mtu neno lake la siri na akifanikiwa kuliingiza kura yake itakubaliwa. Aidha, sanduku hilo litaweza kumpiga picha mtu na kuoanisha na picha yake katika 'chipu' iliyoko kwenye sanduku hilo zikioana hali kadhalika kura yake inakubaliwa.

Sanduku hilo litakuwa linahesabu kura kiouto na kupeleka majibu kwa muda uliopangwa kutokea kwenye video itakayokuwa kwenye eneo la kupigia na kuhesabu kura. Kwa namna hii litakuwa linaondosha haja ya binadamu kuhesabu kura.

Uzuri wa masanduku ya elektroniki ni kwamba ni nchi moja tu inayostahili kuwa nayo. Na nchi yoyote inayofikia kipindi chake cha uchaguzi inaweza kuyaazima kutoka kwa nchi hii. Kutokana na miaka yake na sifa yake katika demokrasia ningelipendekeza India ndio wawe watengenezaji na na wakodishaji wa masanduku hayo.

Kutokana na kurahisisha kazi masanduku elektroniki yatarahisisha pia upigaji kura wakati wowot na mahala popote.

Endapo sanduku la kura elektroniki litakuwepo demokrasia itakuwa imekwepa vigingi vingi vinavyowekwa na wale wasiotaka kuiheshimu na kuienzi na kuwa wakweli, wanaowajibika na watenda haki kwa wanajamii wenzao.

No comments:

Post a Comment